Qari
Murottal Audio
وَالْعٰدِيٰتِ ضَبْحًاۙ
wal-‘ādiyāti ḍabḥā(n).
Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua kwa nguvu,
فَالْمُوْرِيٰتِ قَدْحًاۙ
fal-mūriyāti qadḥā(n).
Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,
فَالْمُغِيْرٰتِ صُبْحًاۙ
fal-mugīrāti ṣubḥā(n).
Wakishambulia wakati wa asubuhi,
فَاَثَرْنَ بِهٖ نَقْعًاۙ
fa'aṡarna bihī naq‘ā(n).
Huku wakitimua vumbi,
فَوَسَطْنَ بِهٖ جَمْعًاۙ
fawasaṭna bihī jam‘ā(n).
Na kuingia katikati ya kundi (la adui),
اِنَّ الْاِنْسَانَ لِرَبِّهٖ لَكَنُوْدٌ ۚ
innal-insāna lirabbihī lakanūd(un).
Hakika mwanadamu kwa Mola wake ni mkataa neema sana,
وَاِنَّهٗ عَلٰى ذٰلِكَ لَشَهِيْدٌۚ
wa innahū ‘alā żālika lasyahīd(un).
Na hakika yeye juu ya hayo ni shahidi,
وَاِنَّهٗ لِحُبِّ الْخَيْرِ لَشَدِيْدٌ ۗ
wa innahū liḥubbil-khairi lasyadīd(un).
Na hakika yeye kwa upendo wa mali ni mkali sana.
۞ اَفَلَا يَعْلَمُ اِذَا بُعْثِرَ مَا فِى الْقُبُوْرِۙ
afalā ya‘lamu iżā bu‘ṡira mā fil-qubūr(i).
Basi je, hajui wakati yatakapo fukuliwa yaliyomo makaburini,
وَحُصِّلَ مَا فِى الصُّدُوْرِۙ
wa ḥuṣṣila mā fiṣ-ṣudūr(i).
Na yaliyomo ndani ya vifua yatakapo tolewa wazi?
اِنَّ رَبَّهُمْ بِهِمْ يَوْمَىِٕذٍ لَّخَبِيْرٌ ࣖ
inna rabbahum bihim yauma'iżil lakhabīr(un).
Hakika Mola wao siku hiyo bila shaka atakuwa na khabari zao wote.